Genesis 18:2-5

2 aIbrahimu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

3Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 4 bAcha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 5 cNiruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.”

Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”

Copyright information for SwhKC